Ni vigumu kuelezea moja kwa moja kujiamini maana yake nini? Lakini mtazamo wa mwanadamu juu ya namna wenzake wanavyomchukulia inaweza kuwa kutafsiri ya neno kujiamini. Ikiwa utajilinganisha na wengine na hatimaye kuhisi aibu, ujue unakabiliwa na tatizo la kujiamini.
Kimsingi kuna mambo mengi yanayoweza kumfanya mtu asijiamini mbele ya wenzake, kiasi cha kujiona duni kwa hili na lile na wakati mwingine hali hiyo humfanya ashindwe kufanya hata mambo ambayo anayajua na kwamba amekuwa akiyafanya kila siku.
Kisaikolojia huu ni ugonjwa ambao unaweza kuathiri uwezo wa mtu kibaiolojia, nikimaanisha kwamba mtu anaweza kuwa si mlemavu wa miguu, lakini akatembea mbele za watu upande upande, anaweza kuwa na akili lakini akajikuta hawezi kuzitumia kwa sababu si mwenye kujiamini.
Kama ilivyo kwa magonjwa mengine, kuponywa kwa tiba, tatizo hili la kutokujiamini nalo linatakiwa litibiwa. Zipo njia nyingi ambazo mtu anaweza kuzitumia kujenga hali ya kujiamini, Kwangu mimi yako mambo 10 ya msingi ambayo mtu akiyazingatia na kuyafanyia kazi anaweza kuondokana na hali ya kutokujiamini.
No comments:
Post a Comment