Social Icons

Sunday, April 20, 2014

MDUDU NDANI YA KOKWA"..BONGE LA STORY KALI YA KIMAPENZI YA WANACHUO...SOMA UELIMIKE...


 Nilikuwa nimemaliza zangu chuo Mzumbe pale, kozi ya BAF (bachellor of accountance and finance) na kufanikiwa kupata GPA nzuri tu ya 4.2. Nilikuwa na matumaini na ndoto nyingi za mbeleni juu ya maisha yangu.


Nilipenda sana elimu na nilitegemea kupata nafasi ya TA (tutorial assistant) chuoni hapo. 



Wakati nangojea graduation ambayo huwa mwezi November, nilienda Dar es salaam kumtembelea dada yangu ambaye alikuwa akiishi huko, maeneo ya Tabata! Naye ndo kwanza alikuwa na mwaka mmoja kazini ila kwa bahati (nzuri?mbaya?…sijui) alipata ujauzito na mshkaji mmoja hivi walisoma naye chuo.

Basi nikawa nakaa naye pale huku nikingojea siku zisonge.


October 06, 2018 siku ya Jumanne:
Siku hii alitakiwa kwenda clinic na kwa vile alikuwa karibu sana na kujifungua hakuweza kuendesha gari ikabidi nimsindikize kwenye zahanati moja pale Tabata nimeisahau jina.


Basi wakati namngojea nikaenda kukaa kwenye mabenchi Fulani pembeni pale kuangalia TV.

Karibu yangu alikuwa amekaa binti mmoja mrembo sana kwa kweli. Sikufahamu yupo pale kufanya nini. Nilidhani na yeye kaja kumsindikiza ndugu yake labda.

Mimi bila hiyana nikaacha kuangalia TV nikaanza kupiga stori za hapa na pale. Tukakonekt vizuri na kuchangia changia mada iliyokuwa inaonyeshwa kwenye TV. Baada ya kama nusu saa dada naye akatoka ndani akaja tuondoke. Nikamwambia dada kama hutojali unipatie namba yako tuzidi kuwasiliana.

Baada ya siku ile tuliendelea kuwasiliana sana tu. Tulikuwa tuna chat mpaka ma saa sita ya usiku na ukizingatia sikuwa na kazi. Aliniambia yupo chuo mwaka wa tatu anasoma Sheria.

KAA NA MIMI…..
Moyoni nilihisi hapa nimepata mtu lakini kama nilivyofundishwa sikuwa na papara ya kumtamkia hayo. Bado ninakumbuka maonyo niliyopewa juu ya jiji la Daslam!

Baada ya wiki mbili hivi tulikutana for lunch posta..enzi hizo break point bado mpya kabisa. Tuliongea mengi about life.

Wiki moja kabla ya graduation nilimwambia naenda zangu Morogoro wiki ijayo hivyo ningependa tuonane. Alikubali na kuja mpaka Tabata jioni. Tulikaa tukala na kupiga stori mpaka mida kama saa sita hivi ucku. Nikatumia mbinu za kimafia kumshawishi kwamba kwenda hostel kwao mida hiyo ingekuwa ngumu ilhali tungeweza kuchukua tu chumba hapo asubuhi arudi chuoni. Of course, strawberry whisky na contessa gin vilichangia kunisaidia kumfanya akumbali. Ila alikuwa amekataa sana mwanzoni.

Tulienda guest moja inaitwa MUNGU ANAKUONA GUEST HOUSE & RESTAURANT. Nikalipa pale tukaingia ndani.
Kazi ikaanza kuomba game ila haikuwa ngumu saaaaana……..

Basi purukushani za hapa na pale za kujiandaa na game na mimi kwa kuwa nilichanganya Contessa gin, zansi na White horse nikasahau kabisaaa matumizi ya kinga. Poor me..!!

Nikaenda zangu graduation November na kurudi. Nikawa nimempotezea kabisa Yule binti kama ilivyo kawaida yetu wanaume baada ya kupata tunda (baada ya kumchezesha ngololo)...

April 15 / 2014 Jumanne:
SMS iliingia : “Ndugu yangu, kama umenichunia sawa ila mbona hata sikuoni tena hospitali?”

Nikashtuka hospitali? Si ikabidi nimpigie!
Ananiambia: “Si pale Tabata sikuoni ukija tena kuchukua ARVs au umebadili kituo?”

Kumbe benchi nililokuwa nimeenda kukalia ile siku lilikuwa la wagonjwa wa UKIMWI nayeye alikuwa akisubiri kuchukua dawa.
Mimi nikamwambia “acha kunidanganya mbona wewe unaishi hostel Kigamboni na ninajua hivyo..yani huko kote hakuna dispensary?”

Akaniambia “wagonjwa wengi hawaendi kuchukulia dawa karibu na kwao kwa kuhofia kunyanyapaliwa hivyo alijua na mimi nipo kwenye foleni ya kuchukua dawa ndiyo maana hakuona umuhimu wa kunilazimisha kutumia kinga cku ile tulivyofuck”
Nilishtuka…nikazimia…ndo nimeamka leo.. 



***** Mwisho ********
ANDIKA MANENO YOYOTE YA FARAJA NA KUMSHAURI MUHUSIKA PAMOJA NA KUWAPA USHIRIKIANO WENZETU WANAOISHI NA VVU …..
TUWE MAKINI JAMANI,UKIMWI UPO NA UNAUA...

3 comments: