Wakati ziara ya dunia ya kikombe halisi cha kombe la dunia ikiendelea kabla ya kukabidhiwa kwa mmiliki wake mpya ambaye ni mshindi wa mwaka huu huko Brazil, maafisa wa China wamekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya 1,000, yaliyokuwa yamedhamiriwa kuuzwa katika kona mbalimbali za dunia
Ikiwa zimebaki siku chache kabla kombe la dunia 2014 halijaanza kutimua nyasi huko Brazil , maafisa wa forodha wa China wamekamata makombe hayo ya dhahabu 1,020 huko katika mji wa Yiwu yakiwa tayari kusafirishwa kuelekea Libya kuuzwa, na kabla ya hapo makombe mengine feki 1,008 yalikamatwa.
Kwa kuyatazama makombe hayo feki yanafanana sana na kombe halisi la dunia.
Kombe halisi la dunia
Kombe halisi la dunia pia lilikuja Tanzania mwishoni mwa mwaka jana 2013.
No comments:
Post a Comment