Social Icons

Thursday, April 17, 2014

UKAWA- KUZUA BARAA BUNGENI.

Bunge Maalum la katiba linaendelea muda huu na leo wajumbe wataendelea kujadili sura ya kwanza na sita ya rasimu mpya ya katiba.

Mh. Sereweji kutoka Zanzibar anasema kuwa muundo wa serikali mbili bado unatufaa,wazanzibar tuna kila kitu hapa Tanzania bara. Anasema wapo bungeni kutafta katiba iliyo bora ya Tanzania na anawasihi wanaosema wataenda Zanzibar kuomba muungano wa mkataba kuwa watakuwa wanavunja sheria.
Anasema mapinduzi yamefanyika Zanzibar unguja ila pemba imepelekwa bendera tu baada ya mapinduzi. Anaunga mkono hoja ya serikali mbili.


Mh. Gaudensia Kabaka, Ameanza kwa kuipongeza tume kwa kazi kubwa iliyoifanya ila akaishauri ilete na yale maoni ya mabaraza ya katiba. Kwa ujumla yeye anapendekeza muundo wa serikali 2 ambazo hazimo kwenye rasimu. 
Anaongezea kwa kusema kuwa serikali ya shirikisho itakua serikali hewa.Kwa ujumla msimamo wa Kabaka ni serikali 2. Mh. Mohamad Sanya, anaanza kwa kusema ni muumini wa serikal tatu na atatetea kwa busara muungano huo.
Anasema Lipumba alionesha jinsi usamehevu wa kodi ulivyo mkubwa hapa na kudidimisha maendeleo. Anasema hataki huu muungano wa sasa,na wanataka muungano utakaoondosha kero kwenye muungano wa sehemu mbili.
Anasema wasilete kisingizio kuwa wazanzibar hawana mafuta na gesi ndo maana wanataka muungano ila wanaweza kujenga nyumba zao bila utegemezi. Anasema wapo hapa kuzungumzia mustakabali wa muungano huu na sio vyama vya siasa.
Anasema wawape nafasi waone watakavyoinua uchumi na hata kusaidia upande huu mwingine wa muungano.Anasema rada kijeshi na mawasiliano ni za muungano lakini baada ya chenji ya rada kurudishwa zanzibar hawakunufaika na chenji hiyo.
Wazanzibar wamechoshwa na muungano huu na wanataka mamlaka kamili ili waweze kuamua mambo yao wenyewe.Anasema kwa muungano huu ccm wataendelea kupoteza kura nyingi visiwani maana wanajali matumbo yao na sio wazanzibar. Zanzibar wana matatizo makubwa lakini hayatatuliwi, anasema kuna watu wa tanzania bara wana uwezo wa kufungua vitega uchumi zanzibar lakini hawaji bali watu wasio na mwelekeo kama wauza karanga ndo wanakuja zanzibar.
Anasema zanzibar wakiwa na mamlaka kamili wanaweza kuibadili zanzibar kuwa Hong Kong ya afrika mashariki.Anamalizia kwa kusema serikali tatu ipo na italeta maendeleo baina ya pande zote mbili. Mh. Diana Chilolo, Anaanza kwa kusema yupo kamati no 12, na anaamini serikali mbili bado zinafaa kufanya kazi katika muungano huu.
Anasema hayaelewa hii rasimu kila akiisoma na kuitafakari mpaka alkafika wakati akakasiri. Anasema labda jaji Warioba kaweka utashi wake na kwanini aweke utashi wake kwenye maslahi ya watanzania kwa kuwaongezea watanzania mzigo wa serikali tatu.
Wizara ya muungano ipo chini ya makamo wa rais aliye mzanzibar,na anasema kweli watu hawa hawajui kero za muungano? Wanazijua ndo maana kati mya kero 27 zimebaki kero saba.
Anamshangaa tundu lissu kuwa alikuwa hawataki wazanzibar hata bungeni lakini anashangaa unafiki wake sasa ni rafiki wa zanzibar na kuwapigania. Anasema kero ya watanzania sio serikali tatu bali huduma nzuri, mishahara iboreshwe na maendeleo mengine.Anawashangaa cuf kwa kutaka kurudisha usultani zanzibar.
Anasema kinachotakiwa hapa ni kuboresha muundo huu wa serikali mbili.Anamuomba makamu mwenyekiti kuwa kwanini hawa wanaowakashifu waasisi wetu kwanini wasisimame mbele ya bunge waombe radhi maana watanzania wana hasira na watanzania hawapo tayari waasisi wao kudharauliwa. 
Anasema watu kama hawa usishangae wakawakana wazazi wao.Anamalizia kwa kutoa mfano kuwa Sitta alipomwoa Magreth alikuwa anaitwa Magreth Simwanza ila baadaye akaitwa Magret Sitta, hoja yake ni kuwa Magret hajamkana baba yake kwa hiyo Tanganyika haijakanwa.
Tunu za taifa anazungunzia kuingiza swala la jinsia maana ni tunu kwa taifa lazima lienziwe 50/50. Mh. Sixtus Mapunda, Anaanza kwa kusema kuwa hataweza kuikana kweli, anaendelea kusema kuwa ukizoea kusema uongo huwezi kusema kweli.
Kuna watu walisema hakukuwahi kuwa na hati ya muungano na kuwakashfu wasisi wetu. 25/4 baraza la wawakilishi lilikaa zanzibar na kambona alihudhulia na aliporudi alipokelewa kalimjee akasema yaliyo tokea. Anaendelea kupangua hoja za Tundu Lissu kuhusu kutokuwepo kwa hati ya muungano, kuhusu kukutana kwa Baraza la Mapinduzi.
Anahoji uhalali wa takwimu za tume ambazo anaona hazikuwa na uhalali kutokana na namna zilivyokusanywa hasa kwa kuacha maoni ya mabaraza ya kata na wilaya. Anamalizia kwa kusema Tunu za taifa zienziwe. Mh. Ali Omar Makame: 
Anazungumzia umuhimu wa kuweka haki za walemavu katika katiba. Hii katiba tuliyonayo imerekebishwa mara 11 lakini mambo ya ulemavu hayamo. walemavu tunataka elimu afya mikopo na ajira na mazingira rafiki. Mimi ni muumini wa serikali mbili. Mimi sikusoma, wasomi watatuelekeza. 
Je serikali tatu gharama zinakuaje? Sisi walemavu tunataka huduma, kwanini hizi gharama za serikali ya tatu zisisaidie wenye ulemavu? Tusaidieni tutoke hapa tulipo sisi walemavu halafu ndo mfikirie kuongeza serikali ya tatu na ya nne. Watu wenye mahitaji maalum katiba itamke ni watu wenye ulemavu.
Vipofu, viziwi viwete ni maneno ya kutudhalilisha. Kubomoa kunasababisha wajane na yatima,mkibomoa watakaopata tabu sana ni sisi walemavu. Anaunga mkono serikali mbili. Mh. Hamis Mnondwa, anaanza kwa kusema ni muumini wa serikali mbili na ana sababu zake.
Anawashangaa wanaoshabikia serikali tatu na anasema kuwa hizi serikali mbili kama zina matatizo basi matatizo yote yanaweza kufanyiwa kazi. Anasema kuna vijana wengi hawana ajira kwanini hizo gharama za serikali tatu zisiwasaidie vijana. Anasema serikali tatu ni kuua muungano wa tanzania bara na Zanzibar.
Tukiongeza serikali ya tatu ina maana tanzania bara na zanzibar bye bye. Sasa hivi zanzibar wanajiuliza jeshi kubwa liko bara, hatuna hela za kugharamia uhamiaji wala hatuna mipaka. Tukiongeza serikali ya tau habari la muungano limekwisha.
Kwanini tusikae tukazungumzia mstakabari wa nchi? Muundo wa serikali tatu ni muundo ambao hauna shida,upo kwa ajiri ya kusimamia majeshi na madaraka. Tanzania haina ardhi, Je serikali tatu itajenga wapi ofisi? Je ni nini kitafuata kama sio mapinduzi? Tutaliwa kodi mpaka ya kichwa na kodi ya kichwa itarudi.
Mh. Zainab Kawawa, Nataka nizungumze na watanzania leo kwanini sikubaliani na serikali inayoitwa ya shirikisho. Nchi ndio inayozaa uraia na kutengeneza utaifa.Jamhuri hiyo ya Tanzania haitoi huduma za afya, elimu na huduma zozote,haiwezekani.Viongozi wa upinzani igeni mfano wa viongozi wa CCM, kwanini chama kimeendelea kuwa imara. 
Nyie hamna utashi wa kuvumilia na kukosoana. Mna hadhi gani ya kuvaa koti linalofanana na wasisi wa nchi hii. Wajumbe wameonesha dhamira ya kuvunja muungano wetu. Hivi ninyi mnaotaka serikali tatu kwa nia mbaya mnaonesha dhamira ya kuuvunja muungano huu,nani asiyejua CHADEMA haina wanachama Zanzibar? 
Watanzania ndio wanaogawa uongozi,waroho wa madaraka ninyi na acheni njia za dezo. Mh. Abubakar, Anasema katiba ni nini? Katiba ni muelekeo wa baadae, katiba ni dira.Katika hii katiba yetu kuna mambo mengi ni dhaifu kwa muungano.Katiba inaonesha ina mamraka tatu, ya Zanzibar, Tanganyika iliyotiwa kwenye mamraka ya muungano. katiba haina misingi ya muungano,ibara ya 98[1b].
Bunge inaweza kutunga sheria na kusema tu itumike Zanzibar, haiwezekani Zanzibar ina wawakilishi wake. Mambo ya nje ina mabalozi kama thelathini kati yao Wazanzibar ni watatu tu, je wazanzibar hawafai.? Kuna mbolea imetolewa na Japanyenye thamani ya billioni 10 lakini Zanzibar haijapelekwa hata mfuko mmoja,je huo ni muungano?
Lililopo hapa Tanganyika imevaa koti la Tanzania ndo maana ikiletwa mbolea inaenda Songea na Ruvuma. Sasa hili koti livuliwe. Sisi Zanzibar tunataka serikali ya shirikisho, lakini lakini tumeimesema serikali moja mbili shirikisho hayafai inayofaa ni serikali tatu basi tumekubaliana nao. 
Serikali tatu ndiyo zitatoa muelekeo wa swala hili. asanteni. Mh. Ramadhan Abdallah Shaabananaongea sasa. Anasema kuwa mambo mengi yaliyoainishwa kama kero za muungano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba tayari yameshapatiwa ufumbuzi.
 Anawataka wajumbe kutumia mjadala huu wa katiba kurekebisha kero zilizopo. Anasema kuwa wanachofanya wapinzani ni kama NDEKWA. kwamba wanatumia madai ya serikali tatu kwa ajenda wanazozijua wenyewe. Kuhusu uwekezaji anasema kuwa wabara na wazanzibari wanawekeza kila upande.
Amezitaja hoteli kama za Sea Cliff ya Subash Patel na Kiwonga inayomilikiwa na watu wa kilimanjaro. Anapendekeza kurejesha mfumo wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano na ugomvi utakuwa umekwisha. Anaunga hoja mfumo wa serikali mbili. 
Mh. Waziri Rajab Salum, anasema ni muumini wa serikali mbili si kwa kufuata mkumbo au kubembelezwa na mtu. Mimi ni msomi nimefanya research na kuona serikali mbili ndizo zitatupeleka mbele.
Huwezi kutengeneza shirikisho bila kuwa na washirika. Zanzibar kukubali shirikisho ni kuigeuza Zanzibar kuwa kama Eritrea na Comoro. Wapinzani wa Zanzibar hawakuanza leo, wapinzani wa uhuru wetu wa 1964 ndo hawa hawa vizazi vyao vinaendelea kuwa wapinzani.
Unapozungumzia Zanzibar unazungumzia Unguja na Pemba. Anasema kuwa wapinzani wa mapinduzi ni hawa hawa wanaopinga muungano hasa kupitia vizazi vyao. Anasema kuwa Wazanzibari wanaotoka Unguja, wana muingiliano na watu wa bara huku wa Pemba hawana muingiliano wa kidamu zaidi ya ule wa kibiadhara. 
Wanaotaka Serikali tatu wanataka kuvunja muungano na kuchukua maduka yao na kupeleka Pemba. Nature ya binadamu yoyote anapoambiwa ukweli lazima akasirike. Kwa vile naunga mkono serikali mbili napendekeza rais wa jamhuri na makamu na rais wa Zanzibar na makamu rais wa kwanza na wa pili wa Zanzibar washirikishwe kwenye jamhuri na watambuliwe kuulinda muungano wetu.
 Tupo hapa kama taifa moja,tuache ushabiki tuambizane ukweli. Mh. Issa Gafu, Anasema Naunga mkono mapendekezo ya wengi ya kamati namba 11. Tuendelee kubaki kwenye mfumo wa serikali mbili.
 Ulinzi na usalama zinahitaji fedha nyingi,usalama na ulinzi upo kwenye serikali ya tatu ya muungano ambao hauna vyanzo vya mapato. Zanzibar imetuchukua miaka 40 bila hawa wanasiasa kuyatambua mapinduzi tukufu ya zanzibar. kama anaweza kubana uhuru wako hawezi kukupa uhuru wa kuuukubali muungano.
Tatizo la zanzibar sio mfumo wa serikali bali uchumi. vinginevyo tukitaka serikali tatu ina maana tunataka kuuvunja muungano jambo ambalo sipo tayari kufanya hivyo. Faida za muungano zipo nyingi tu. Bila muungano kusingekuwepo na sherehe za mapinduzi, maadui wa mapinduzi bado wapo.
Shindanisha maendeleo ya miaka 200 tuliyo tawaliwa na miaka 50 ya muungano. Hatukua na mtaalamu hata mmoja lakini sasa hivi tuna wataalamu wengi. Nawaomba wabunge tukisimama tujisemee sisi wenyewe sio kuwasemea watanzania eti wamewatuma.
Mh. Tundu Lissu anasema, Naomba nianze kwa kujibu vihoja. Kuna kihoja kinasema Tundu Lissu amemtukana baba wa taifa.1995 baba wa taifa alihutubia Mbea akasema, asiyekubali kukosolewa hawezi kuwa kiongozi bora. Baba wa taifa alikuwa binadamu hakuwa Mungu wala malaika alikuwa binadamu na hajawa mtakatifu bado.
Baba wa taifa alishawahi kuunga mkono vita ya BIAFRA wakliotaka kujitenga na Nigeria. Anasema kuna watu walikimbia ccm na kukimbila nccr Mageuzi na walirudi baada ya Mwl Nyerere kufariki.Hati ya makubaliano ya muungano haupo.
Tumeoneshwa sahihi nenda ulinganishe. Leteni hizo sahihi hapa tuwaonesheni mlivyo waongo. Zanzibar haijawahi kuridhia muungano mpaka kesho kutwa. Kama mashariti ya muungano hayajatekelezwa kwa miaka 50 ni halali?   
Muundo wa shirikisho wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Nyalali, Kisanga, Walioba na wananchi ndo unafaa. Ndivyo alivyo pendekeza Mwakyembe miaka 20 iliyopita. Rais wa Tanzania Kikwete sio mkuu wa Zanzibar. 
Katiba ya Zanzibar inasema rais wa Zanzibar atakua ndio rais mkuu, na mkuu wa vikosi maalum, Ibara ya 26(1) ya katiba ya Zanzibar. Haya sio maneno ya Tundu Lissu ni maneno ya katiba ya Zanzibar.Nani anaye weza kusema sisi ni nchi moja. Kikwete akienda Zanzibar anayepigiwa mizinga ni Shein, Kikwete akiwa mbali kabisa. 
Mkiwa na rais magogoni mwingine mmnazi mmoja wakipishana itakuaje? Tutengeneze utaratibu mpya baada ya miaka 50 ya kudanganyana. Tusipochukua hatua za haraka mbele ni giza tupu. Watakaoanzisha muda si hawa wanaoanzisha katiba mpya bali ni wale wanaofumba macho wakati mambo yakiharibika.
Mh. Benard Membe anasema, Huu ni muungano wa pekee na wa pili duniani uliodumu ukifuatia ule wa Canada.Tunaweza kuunda muungano wa nchi hizi mbili lakini serikali ya Tanganyika itaua serikali ya muungano na shahidi atakua serikali ya Zanzibar. 
Tume ya Warioba italaumiwa kwa kupaga mauaji hayo. Naungana na CCM kwamba jibu pekee ni serikali mbili. 1988-1990 huu ndo ulikuwa ubishi Urusi. Kwanini tusijifunze kwa Urusi iliyokufa baada ya mwaka mmoja?.
 Nawauliza mpo tayari mkubali Zanzibar na Tanganyika msikusanye kodi, kodi ikusanywe na jamhuri? {wabunge wameitikia ndio} Serikali gani duniani inayoendeshwa bila kodi?Mifano niliyoitoa ya Urusi, Spain na Ujerumani inatosha.
Tukiunda serikali tatu itaua muungano.Hakuna nchi duniani ambayo inatukana wasisi wake. Na bunge litakua wa mwisho kuwatukana waasisi. Tuna tatizo la kujifanya wajuaji.Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayeenda mbele ya hadhara na kuwakejeri.
Hati ya muungano nimeiona na ni halali na ndiyo mtakayoiona hapa na haikuchakachuliwa. Mh. Khalifa Khalifa anasema, Kwanini tumefika mahala kwenye chombo kama hiki baada ya kuleta hoja tunatukanana? woga huu wa nini? 
Mimi tume ya Warioba naiunga mkono. Hawa walikua 30 sisi tupo 600 na kitu.Warioba alisema tutenganishe mamraka ya muungano ya Tanganyika na Zanzibar yakae mbali. Je ni halali mabolozi kutoka Zanzibar wawe wanne tu? je Zanzibar haifai kupata kiongozi mkuu jeshini? Tusikie humu ndani tukatukanana bure hadi kuwatukana viongozi wa nje. 
Mtu anaongea ubaguzi wa Unguja na Pemba mnampigia makofi. mtu anakuja huku anajisifia kwa kabila lake mnampigia makofi kama huyu.
Mh. Amon Mpanju anasema; Yanapotokea mafuriko kama haya walemavu tunataabika,yanapotokea mabomu walemavu tunataabika. Sijapendezwa na kauri ya viongozi wanaosema kwamba kama serikali tatu haziruhusiwi tupo tayari kwa lolote.
mimi ni mwenyekiti wa walemavu nina wafuasi pia, kuna wakulima wana wafuasi pia. Watanzania wenzangu hatunabudi kuwasusa watu wa namna hii. nawaomba sana vijana tusiwaunge mkono. Jussa alinambia anapuuza taarifa na mimi ananipuuza. 
maneno haya yaliwaumiza walemavu. Tusimguse Mungu machoni kwani hakuna aliye amua kuwa mlemavu.Ibara ya nne kuna mapendekezo yameletwa nami nayaunga mkono. 
ligha ya alama na lugha ya alama amguso itakua ni ligha ya alama kwa watu wasio ona. haya mabadiliko nayaunga mkono. Nashangaa sana wanaanza kuhoji na kubeza uhalali wa huu muungano hasa tundu lisu. huu muungano sio wa wanasheria ,huu muungano unatambulika hadi UN.
huu muungano una matatizo lakini tunaweza kuyatatua kwa kupitia muundo wa serikali mbili. uanasheria wenu usiwe kero. Tuache kupotosha watanzania. serikali tatu ni kaburi la Muungano. 
tuache kuhubiri ubaguzi la sivyo zanzibar watagawana mikoba na huku bara tatagawana mikoba. Tuache kuwapa nafasi wazandiki na wanafiki wa nchi hii. wanasema wana watu wakati hawana watu kalenga na chalinze ilionesha.
Mh. Jussa anasema, hawezi kujibu matusi kwani akili ndogo ndio inayojadili watu badala ya hoja. Nasimamia matakwa ya Znz, tunataka mamlaka kamili.
Anasema wanaosema kuwa serikali mbili zitaleta maendeleo Zanzibar mbona zimeshindwa kuyaleta kwa miaka 50? tume ya Amina iliorodhesha matatizo lukuki ya serikali na wote walikuwa CCM Mh. 
Yahya Kassim, anasema katika upotoshaji huu kuna haja ya kuzungumza ili wapinzani waelewe.Wengine hawaelewi ukweli ulivyo.
Zanzibar imepatikana kwa mapinduzi na bara kwa kura na waliowaondoa hawapo.Anasema zanzibar kweli wana uwoga,mana siku ya uchaguzi pia ni waoga kusema kuwa mwisho wa utawala wa weusi ni mwisho.
Kuja waarabu zanzibar wanakuja wanasema ardhi hii ya baba yangu anaitaka, je tutaishi wapi? Anasema yeye ni muumini wa serikali mbili kwasababu katika rasimu hii hakuna mtu zanzibar aliyesema anataka serikali tatu, zanzibar walisema wanataka serikali mbili na ya mkataba.
Mh. Fathyiha Zahara Salum, anasema kuwa wazanzibari walichoka kuuliwa ndo maana wakaamua serikali ya umoja wa kitaifa. Kila siku watu wanauana na kuchinjana humu humu Tanzania chini ya s2. tusitishane.
Mheshimiwa sana Zitto Kabwe, Anasema kuwa mchakato huu ambao ulipaswa kujenga maridhiano, unajenga hali ya ubaguzi na kuna lugha na kauli za kibaguzi zinatoka huku watu wakishangilia.
Anasema kuwa tujadiliane kwa hoja, watu wajadiliane na wamue na kitakachoamuliwa ndicho kitakachoenda kwa wananchi Anasema kuwa hakuna uhusiano wa muundo wa muungano na uimara wa serikali.
Muundo wowote wa Muungano, uwe wa serikali 1, 2 au 3 bila maridhiano utavunjika tu! Hakuna utafiti wowote wa kitaalam unaothibitisha kuwa Serikali tatu zitaongeza gharama! Tunaweza tukawa na rais mmoja wa Serikali kuu na wakuu wa nchi washirika.
Kuna jumla ya 2.3tril kila mwaka hazikusanywi kama mapato ya Taifa! Tunao uwezo wa kuendesha aina yoyote ya Muungano! Anasema kuwa tunao uwezo wa kuendesha muungano wowote kama tukiamua kukusanya kodi ipasavyo. 
Zitto anasema kuwa ikiwa muungano utavunjika, gharama za kuzilinda nchi zake ni kubwa zaidi kuliko gharama za mfumo wa serikali tatu. Mh. Ritha Mlaki, Anasema anapendekeza S2Mh. 
Serukamba, CCM Tunalo jukumu la kulinda Muungano huu. Muungano utakuwa salama mikononi mwa CCM!Wapo wanaosema CCM tunang'ang'ania s2, ni kwamba sisi tuna dhamana.
serukamba: Lissu alisema uongo wa miaka 50 umefika mwisho. Mwl ameleta uhuru na amani na muungano Mnataka kuudumisha Muungano gani ambao mnadai hati zake zimegushiwa? Mnaotaka s3 mnasema mnataka muungano imara lakini mnataka kuvunja muungano.
Anasema Jussa anataka Zanzibar yenye Mamlaka kamili. Anamaanisha TUUVUNJE MUUNGANO!
=============== ===============
Makamu mwenyekiti anatoa matangazo ya wageni wa wajumbe wa bunge maalum la katiba pamoja na wageni wengine waalikwa. Anasema amepokea hati ya makubaliano ya muungano na ni certified copy.
Anamkaribisha mh. Wassira aweze kutoa neno kuhusu hati hiyo. Mh. Steven Wassira, anasema hati hiyo ipo na ni halisi na ipo katika hali nzuri hata baada ya kusainiwa miaka hamsini iliyopita.
Anasema kuwa Tundu Lissu na wenzake walikutana baada ya kujua hati ipo na wakakubaliana waseme saini ya Sheikh Karume sio ya kweli. Anasema watanzania tujihadhari na mawakala wa shetani.
Anasema waasisi wetu wametukanwa sana mpaka kuitwa madikteta na hali hii haivumiliki kwa watanzania wote.
Anasema heshima ya waasisi wetu hailindwi na vyama bali inalindwa na italindwa na watanzania wote.Makamu mwenyekiti, Bunge litaendelea Saa kumi jioni.Anasitisha kikao cha bunge maalum la katiba.
======== ===============
Bunge Maalum la Katiba, kikao cha jioni Mh. Anaanza kwa kuunga mkono maoni ya wengi ambayo inatambua uwepo wa serikali mbili.
Anasema zanzibar kuna makundi mawili yanayotaka mkataba na serikali mbili.Sababu za kuunga s2 ni kuwa muungano huu ni kuna kero za muda mrefu na anasema kuwa kuna kero zishatatulika.Serikali ya tatu ya nini wakati kero zinatatulika.
Anasema kuwa s3 haijaja lakini tayari ina kero 6,yanini kuwa muungano wa s3 ambayo tayari ina kero sita wakati kero za s2 zinatatulika. Anasema cuf imefika bara na kumezwa na ukawa,wametoka zanzibar na asilimia 65 ya serikali ya mkataba lakini walivyofika bara wakamezwa na chadema.
Anasema chadema imewapa cuf majina tofauti na cuf wamejisahau kuwa chadema ndiyo inayoibomoa zanzibar.
Anasema amiri jeshi mkuu wa tanzania ni mmoja na ni rais wa JMT hivyo tundu lissu asipotoshe. Anasema miaka hamsini hii ya muungano hawapaswi kustuka maana mtu mzima hatishiwi nyau.
Mh. Mch. Ernest KadivaAnaanza kwa kumshukuru Mungu.Anasema wanatakiwa kuunda katika ya wananchi wote na yenye misingi madhubuti ya kusimamia nchi kwa muda mrefu.
Anasema taifa linaeza kuporomoka muda wowote kama haina msingi ulio imara na hivyo msingi lazima ulindwe. Anasema kuwa ili taifa liweze kuvunjika lazima ikatwe mizizi imara ya msingi wa taifa hivyo taifa litatetereka.
Anapendekeza kuwa JMT ni nchi inayomtambua Mungu, Isiyo na dini na isiyoruhusu uchafuzi (kashfa) za kidini.Anasema dini ni msingi imara wa ustawi wa nchi.
Anasema kama wosia wao bado una mantiki katika muundo huu wa serikali mbili basi bora uenziwe.Wananchi wanataka kuona uchumi ulioimarika na mfumo watakaoutaka basi uhakikishe unazingatia na namna ya kuimarisha uchumi ambacho ndo wananchi wanachotaka kuona.
Mh. Prof LipumbaAnasema yeye ni muumini wa dini ya mwenyezi Mungu hivyo ni muumini wa mapendekezo yaliyoletwa na tume ya Warioba.
Anamnukuu Lukuvi alivyoenda kanisani na kuwaasa waumini waupinge muundo wa S3 lasi hivyo nchi itataliwa na jeshi,anasema Lukuvi aliwasilisha maoni ya Waziri mkuu.
Anasema km zanzibar wangetaka muundo wa s1 moja basi wangekuwa na muundo wa serikali moja lakini wazanzibar hawati muundo huo,anasema wanataka muungano utakaokuwa na maridhiano.
Anasema wanahitaji katiba itakayokuwa sawa kwa wananchi wote maana ndo msingi ulioachwa na mwl Nyerere.
Anasema ni fedhea kwa waziri kwenda kusema kanisani kuwa cuf zanzibar wanataka muungano utakaoifanya zanzibar kuwa nchi ya kiislam. Anasema watatumiaje bajeti kubwa kukarabati ukumbi wakato wanajua katika hawaitaki.
Anasema wamechoka ubaguzi na kudharau maoni ya wananchi.Anasema watu wote wanaokubaliana na maoni ya wananchi wanaondoka bungeni na kuwaacha wao wajadili katiba wanayoitaka.
Wabunge wengi wameondoka ndani ya ukumbi wa bunge na makamu mwenyekiti anasema kuwa wakati wanaanza kikao cha bunge kolamu ilikuwa imetimia hivyo kanuni inawaruhusu kuendelea na kikao.
Mh. Nyangwine Nyambari, Anasema kuwa tume ilikuwa ishapanga maoni yao binafsi na sio maoni ya wananchi.
Anasema wajumbe walioondoka ni wanafiki wakubwa na wamemsaliti mwalimu Nyerere. Anasema historia ya zanzibar inapotoshwa sana kwa makusudi, ananukuu kitabu fulani na kusema kilichoandikwa ni uongo na kinapotosha historia ya zanzibar.
Anasema mwl nyerere amesaidia nchi nyingi kupata uhuru hivyo hawezi kuwa na njama hasi juu ya wanachi. Anasema kwakuwa wapinzani wameondoka hivyo wao waliobaki waongozwe na utashi kuweza kufanya yaliyo mema kwa wananchi.
Anapendekeza kuwa alama za taifa waongeze nembo ya simba maana simba ni mkali na watoe ya twiga aliyekaa kizembe. Anazungumzia pia kuhusu tunu ya taifa na kupendekeza vipengere vya kuongezwa.
Anasema wale wanaotishia kuwa bila serikali 3 hakuna utawala bora na wanatumia nguvu nyingi na ubabe basi wapuuzwe hawana jema kwa wananchi.
Mh. Ole Nasha,Kwa ujumla anazungumzia masuala ya ardhi na wafugaji na ugomvi unaosababishwa na sera mbaya ya ardhi na kupelekea mauaji baina ya wafugaji na wakulima. 
Anasema Tz imejaliwa rasilimali za wanyamapori lakini haziwasaidii wananchi walio wengi.
Mh. Anaungana na walio wengi kwa kuendelea kuwepo serikali mbili.Serikali mbili ndiyo imeleta amani na maendeleo ya Tanzania hivyo haungano na muundo wa s3. Anasema wapinzani wanapotosha kwamba s3 ndiyo italeta maendeleo hapa hilo ni uongo.
Anasema kuimarisha muungano sio lazima kuwe na serikali tatu hizi mbili zinatosha.
Yapo mengi ya kuyafanyia mabadiliko ambapo kama wajumbe waliotumwa na wananchi kuibadili katiba itakayoleta maendeleo kwa wote. 
Anasema wapinzani hawawatakii muungano na kuwatakia mema wananchi wa tanzania. Mh. Mwagachi,Anasema amesononeka sana wapinzani kutokaa kusikiliza mjadala huu hivyo hatendi haki kwa wale waliokuja kuwawakilisha.
Anasema waasisi wetu wanastahiki heshima kubwa pamoja na kuwa na mapungufu machache,ila walifanya yaliyo mema hapa. Anasema ameshangaa kuwa kuna watu wanasema kuwa mwl Nyerere sio mtakatifu wakati dunia nzima ipo kwenye mchakato wa kumfanya kuwa mtakatifu.
Anasema waasisi wetu kwenye Berlin conference waliwasuta wale watu kuwa waafrika wanaweza kujitawala bila tatizo.
Anaunga mkono serikali mbili na washindane kwa hoja kutetea maoni yao na sio kwamba nataka serikali mbili au tatu bila hoja. Anasema hawawezi kuwapa watanzania mzigo wa kuendesha mzigo wa watu miliono 43 alafu wawaongezee mzigo mwingine wa serikali tatu,yaani marais watutu,waziri wakuu watatu, makamu wa rais watatu pamoja na familia zao
Katika mfumo huu wa vyama vingi vyama vinakwenda kwa wananchi kuomba sera zao na ndiyo wananchi wanazotaka na sio sera zitakazoleta mkanganyiko.
Viongozi imara wanatetea umoja siku zote,muungano na umoja umedumu kwa miaka 50 na tunaweza kuongeza miaka mingine mingi kwa kudumisha muungano huu wa serikali mbili.
Mh. Cyril Chami,Anazungumzia kuhusu takwimu za watu watu waliotoa maoni katika tume ya Warioba.Anasema takwimu zilizotolewa zinaondoa uhalali wa kutumika maana kuna maoni ya watu wengi yameachwa.
Badala Tume ikaja na takwimu kwamba watu walio wengi walipendekeza muundo wa s3.Taasisi ya CCM yenye wanachama 6,500,000 wapo wengi na maoni yao hayajachukuliwa eti tume inakuja na watu 47 elfu eti ndio wamependekeza s3,haoni taasisi ya ccm ni kubwa kuliko hao wanaotaka s3.
anawaomba watu wote wanaopendea mema nchi hii kuwa macho na hao wapinzani wanaotaka kuharibu muungano huu kwa kupotosha.
Mh. Zainab Gama, Anasema wapinzani walitaka kuondoka wakisingizia hati ya muungano hakuna, hati imekuja bungeni wamekosa kisingizio na kuamua kuondoka.
Anasema wao waliobaki baada ya wapinzani kuondoka wamebaki wengi hivyo anaomba wahakikishe muundo wa s2 unasimama. Anazungumzia takwimu za maoni ya tume ya jaji warioba na kuyakosoa kuwa ni ya uongo hayana ukweli.
Anasema kuwa tume imedanganya kuwa watu wengi wanataka serikali tatu,anasema tume ina wasomi,majaji lakini wameshindwa kukotoa hesabu ndogo.
Anasema tume imekula rushwa hivyo inataka kusaritisha nchi hivyo isikubalike kamwe. Anasema kuwa wao kundi 201 waliokuja kuwakilisha wananchi wanajua kuwa wamekuja kuwakilisha kweli.
Anaomba wakae na wabadilishe ili rasimu iwe na nguvu ili wavuvi,wakulima na wanawake wawe na nguvu. Anamsihi rais Kikwete kuwa hawa waliotoka wasiende kwake kumpigia magoti maana wamemsaliti na posho wanyang'anywe.
Mh. ZenaAnasema yeye ni muumini wa s2 ya mapinduzi ya zanzibar na jamhuri ya muungano wa tanzania. Anasema baada ya miaka hamsini pemba na unguja imepata maendeleo kama elimu bure, afya na barabara hivyo muungano huu kwake una maendeleo.
Anasema wapinzani wanasema wanabanwa kwenye hizi serkali mbili lakini wataendelea kubanana hapahapa kwenye muundo huu wa s2. 
Muungano wa s2 ni halali kweli tena halali ya juu.Anasema anayoitaka zanzibar yake ataipata huko lakini sio hii ya muungano. Rais Shein kafanya mambo mengi zanzibar imeng'ara.
Anawapongeza waasisi wote na wanaowatukana waasisi hawa hukumu yao ipo.Anasema mh. Kikwete akija zanzibar sio kweli anapanga foleni,huo ni uongo anakuja ikulu kwa raha mstarehe na anafurahia.
Kikwete akienda kule kuna sheria zake na hata Shein akija bara kuna sheria zake hivyo upinzani waache upotoshaji.Anasema pemba na unguja wote wanataka serikali mbili na huu mwaka wa 50 hakujatokea tatizo lolote.
Anasema zanzibar watatue matatizo yao na km wakishindwa basi waombe msaada upande wa pili wa muungano.Mh. Faida BakaryAnaanza kwa kusema wamewashinda kwa hoja wapinzani mpaka wakaamua kutoka.
Mimi ni muumini wa serikali mbili vile vile muumini wa CCM ambayo inaongoza muungano huu wa s2. Anasema anaunga muungano huu maana una faida nyingi ambazo ameziona tangu azaliwe.
Muungano huu umeasisiwa na hayati Karume na Nyerere, umeleta muungano,amani na upendo eti baada ya miaka hamsini wanataka tuuvunje!! Wazanzibar sasa wako bara na wabara wako zanzibar wamedumisha mshikamano tunataka nini tenaaaaa!!
Ananukuu kifungu kinachoupa uhalali muungano huu, uliondikwa na mwl Nyerere.Anasema tume ya warioba ilipewa rejea sasa iweje leo waje na maoni yao na kuunyong'oa huu muungano? Wapinzani pia walaaniwe kwa kutaka kuuvunja huu muungano na Mungu atawalipa.
Anasema kule pemba kuna miradi mingi mikubwa na yote hii miradi ya muungano iliyotuunganisha Anasema anawakilisha wananchi wa pemba na wananchi wa pemba wanataka serikali mbili na sio tatuuu!!
Mh. Amina Mweta,Anapendekeza kuwa uhujumu uchumi na ujangili pamoja na dhuruma zote ziondolewe nchini anapendekeza maneno haya yaingie kwenye katiba. Anasema katika tunu za taifa liongezwe neno demokrasi na pia usawa wa jinsia.
Muundo wa muungano ni vizuri watanzania wakaelewa historia fupi ya tanzania hata tume kabla ya kuandika rasimu iliangalia historia taifa letu.
Anasema tume imekiri pia kuwa jina tanganyika tulikuja kupewa na wakoloni waliotutawala, hapo mwanzo tulikuwa pamoja na rwanda na burundi. 
Anashanga kuwabeza waasisi ambao walituletea muungano hu.Anasema pia kuleta muundo wa s3 moja kwa moja ni kuuvunja muungano, hivyo anashangaa mapendekezo. Anasema kuongeza s3 ni matatizo mfano maraisi wa tanzania,zanzibar na muungano watoke vyama vitatu tofauti kweli patakalika,mfano tukiangalia hapa bungeni jinsi ilivyo.
Anasema wananchi wanapenda serikali mbili ziendelee kuongoza nchi hii.Mh. Jaji Simai Jaji, Anasema serikali tatu ni misingi ya kuvunja muungano maana haamini kuwa hawa wote hawaamini kumwa s3 itavunja muunganoAnasema kuwa maoni ya serikali tatu sio ya wazanzibar bali wanasiasa waliowarubuni wananchi ambao hawajui wataenda kuzungumza kitu gani.
Anawashangaa hao wanasiasa kuja na mfumo wa s3 na huku wakijua chini ya mfumo huo mamlaka kamili ya zanzibar hayawezi kupatikana.Wamewadanganya wananchi.
Watu hao wamekuja na maono ya muungano wa mkataka na hilo limethibitishwa na mjumbe mmoja aliyeongea asubuhi. Anasema hilo haliwezekani na wao ndio wazanzibar wenyewe.
Muungano wa s3 ni rahisi kuvunjika maana zanzibar haina uwezo wa kwenda kugharamikia serikali ya tatu,hawana uwezo huo kamisa na niz mzigo ambao hawana haja nao.
Anawashukuru wabara kwa uvumilivu pamoja na kuambiwa kuwa wabara wamevaa koti la muungano,anasifu wana haki hiyo maana wao wamechangia asilimia kubwa ya rasilimali.
Jusa alisema kuwa endapo s3 haitopita basi watawaambia wananchi kuandamana kudai muungano wa mkataba na anasema kama muundo huo wa s3 tatu kama umeshindwa kupita hapa bungeni basi hata huo wa mkataba hauwezi kufanikiwa.
Anamalizia kwa kusema s2 ndio suluhisho pekee la kuufanya muungano huu undelee kudumu. Bila s2 basi muungano huu tutauzika.
Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, Anasema ni mjumbe kati ya wajumbe 201 na ni mwakilishi wa taasisi ya Anglikana na ameagizwa na askofu kusema haya,Muundo wa mamlaka kamili ya tanzania yawe ya muungano wa s2.

No comments:

Post a Comment