Social Icons

Wednesday, April 16, 2014

MAKAHABA WANASWA NA KUPEWA KICHAPO BAADA YA KUJIUZA WAKIWA WAMEVAA NGUO ZA JESHI!



HAWA NI WANADADA, WAKAZI WA DAR ES SALAAM WAFANYAO UKAHABA KAMA KAZI YAO YA KUJIPATIA KIPATO NDANI YA JIJI NA KUENDESHA MAISHA YAO.


WAREMBO HAWA HUFANYIA BIASHARA ZAO KATIKA VIWANJA VIKALI VIKALI VYA DAR ES SALAAM ( MAJINA YAMEIFADHIWA) NA HIVYO KUKUTANA NA WATU MBALIMBALI, KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI ZA DUNIA HII NA KUPATA MKWANJA MNONO KUTOKANA NA UZURI WAO!!

BIASHARA YAO HII JANA ILIONEKANA KUVUKA MIPAKA NA KUINGILIA SEKTA MBAYA, YAANI SEKTA YA WAJEDA, WEZEE WA TIFUTIFU NA HIVYO KUKIONA CHA MTEMAKUNI!!

TIFU LA JANA USIKU LILIKUWA MATATA SANA PALE WALIPOKUTANA NA WAJEDA WAKIWA KWENYE HARAKATI ZAO ZA KULINDA AMANI YA TAIFA, NA HIVYO KULA MKONG`OTO USIOWEZA KUSIMULIWA KWA MANENO MATUPU. UKONG`OTO HUO ULIAMBATANA NA VIJIADHABU VYA HAPA NA PALE, UNAJUA TENA ADHABU ZA WAJEDA!!

WAKATI WANAHOJIWA , WAREMBO HAWA WALIDAI,

"TUNATUMIA NGUO HIZI ZINAZOFANANA NA ZILE ZA JESHI ILI TUWEZE KUWADHIBITI WATEJA WETU KWANI, INAONEKANA KUWA WATU WENGI WANAWAOGOPA SANA WAJEDA.....WATEJA WENGINE NI WAKOROFI SANA, KWA SABABU HUWA WANAKULA MZIGO LAKINI KULIPA HAWATAKI AMA WANAANZA KUBADILISHA KIWANGO CHA BEI TULIYOKUBALIANA KABLA YA KUPEANA MAMBO!!!"

KISA CHA TIFU LA JANA KINAFANANA SANA NA KISA CHA WATOTO WANAOKAA MAENEO YA KARIBU NA KAMBI YA JESHI YA MABIBO WALIOKUWA WAKILA MABUNGO HUKO JESHINI MARA KWA MARA. KAMA ILIVYO ADA, ZA MWIZI NI AROBAINI, WATOTO HAO WALINASWA NA WAJEDA NA KUPEWA ADHABU YA KULA UGALI WA UNGA KILO SITA, WATU WAWILI! CHA KUCHEKESHA WATOTO HAO WALIKUWA WANACHOTA TONGE LA UGALI ULIOKUWA UMEWEKWA KILOMITA NANE KUTOKA KWENYE BAKULI LA MBOGA, NA KUANZA SAFARI YA KWENDA KUCHOVYA KABLA YA KULILA TONGE HILO. 

WALIPASWA TENA KURUDI KWA SPIDI KALI KUCHUKUA TONGE LINGINE NA KURUDI MBOGANI KWA KASI ILEILE!!!!

No comments:

Post a Comment