Habari kutoka nchini Poland ni kwamba goli la mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo lilimsaidia mtoto aliyepoteza fahamu kwa muda wa miezi mitatu kurudiwa na fahamu zake.
David Pawlaczyk aligongwa na gari akiwa anaendesha baiskeli yake na kupata majeraha makubwa kichwani mwezi August mwaka jana.
Mtoto huyo mwenye miaka 14 alipelekwa hosptali lakini akapoteza fahamu (coma), kama ilivyoripotiwa na gazeti la Poland la Fakt.
Wazazi wake waliambiwa kwamba matibabu ya sauti (sound therapy) ndio yalikuwa matibabu mazuri katika kumtibu mtoto wao na wakapewa maelekezo kwamba wawe wanamuekea sauti ambayo atakuwa anaifahamu.
David alikuwa shabiki mkubwa Real Madrid na wazazi wake walimuwekea matangazo ya radio ya mechi za Real Madrid ikiwa ni moja ya mbinu za kujaribu kumtibu.
Wakati Ronaldo alipofunga goli wakati wa mechi ya kogombea kucheza kombe la dunia dhidi ya Sweden mnamo mwezi November 2013, David alikuwa akisikiliza matangazo ya mechi hiyo na baada ya goli la Ronaldo, mtoto huyo akaamka kutoka kwenye ‘coma’.
Vyombo vya habari vya Poland viliripoti tukio hilo na likamfikia Ronaldo na mchezaji huyo akawaalika David na wazazi wake kwenda kuangalia mchezo wa Madrid dhidi ya Dortmund.
No comments:
Post a Comment