Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, amepinga mfumo wa muungano wa serikali tatu unaopendekezwa na Rasimu ya Katiba na ameunga mkono hoja ya kudai serikali mbili.
Akichangia mjadala wa sura ya kwanza ya rasimu bungeni, Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa TLP, ameongeza idadi ya wapinzani wachache wanaounga mkono serikali mbili, zinazopendekezwa na CCM.
Alifananisha wanaopendekeza serikali tatu na upepo ambao ukipeperushwa hutoweka ghafla.
Mrema alisema amekuwa Ofisa Usalama wa mikoa tofauti nchi na alifanya kazi kwa karibu na Sokoine, akasema Mkataa pema pabaya panamwita na asiyejui kufa, achungulie kaburi. Alitaka Wazanzibari wasishabikie serikali tatu kwani hali ya usalama nchini siyo nzuri na kwamba hali ni mbaya zaidi kwa upande wao, eti wananyemelewa. Waliokimbia Mapinduzi ya Zanzibar, walielezwa na Mrema kuwa hawako mbali, wakati wowote mgogoro ukianza warejee visiwani Pemba na Unguja.
Wakati wote, hotuba yake ilitawaliwa mashangilio ya wajumbe wa CCM na alisema mfumo wa serikali tatu ukikubalika, jeshi litatwaa madaraka ndani ya mwezi mmoja tu.
Mrema aliwashauri Wazanzibar wajiulize juu ya walikotoka Uamsho na kiini cha mauaji ya raia wasiyo na hatia, wakiwamo Mapadre wakipata majibu wataona kwanini hawatakiwi kuunga mkono serikali tatu.
No comments:
Post a Comment